BUDECO yatoa tamko la kulaani unyama uliofanyika wilayani Busega, Simiyu
Hapo tarehe 12/09/2014 JUMUIYA ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) ililaani vikali tukio la kuporwa pesa kwa walimu na kubakwa kwa mwalimu wa kike wa shule ya sekondari Kishamapanda iliyoko wilaya ya Busega, mkoani Simiyu.
Tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka huu, ambako watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi waliokubuhu walivamia nyumba ya Mratibu wa Elimu Kata, Samwel Mkumbo na kumpora shilingi milioni 18 kabla ya kwenda kwenye chumba cha mpangaji wake wa kike ambaye pia ni mwalimu na kumpora shilingi 50,000 na kisha kumbaka kwa zamu.