Ijumaa, Julai 05, 2024

Sekta Utalii:

  1. Kuunganisha waendesha biashara ya utalii katika mkoa wa Mwanza ili kuweza kulitangaza eneo la ukanda huu kwa pamoja.
  2. Kuongeza utangazaji wa utalii katika mwambao wa ziwa Victoria ili kuongeza biashara ya utalii katika eneo lililopo jimboni.
  3. Kuvutia uwekezaji wa mahoteli katika mwambao wa ziwa Victoria na pembeni mwa vilima jimboni, na kuhamasisha michezo ya majina na meli za starehe.
  4. Kubainisha mambo ya kale na shughuli za kiutamaduni zilizopo jimboni zinazofaa kutumika kama kivutio cha utalii.
  5. Kufundisha wananchi ili waweze kushiriki katika biashara ya utalii.

Sekta ya Ufugaji Nyuki:

  1. Kuleta waelimishaji wa ufugaji nyuki toka TAWIRI/SIDO/Idara ya Misitu na Nyuki.
  2. Kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki Badugu, Nyaluhande, Ngasamo, Kiloleli, Mwamanyili, Kabita, Shigala, Igalukilo, Malili, Mkula na Kalemela.
  3. Kujifunza na kusindika mazao ya nyuki.
  4. Kubaini na kuvutia masoko ya mazao ya nyuki (mf. Mohamed Enterprises kwa ajili ya nta).

Sekta ya Mazingira:

  1. Kuhamasisha upandaji miti kama zao la biashara – kwa familia na taasisi (kushirikiana na Tanzania Tree Seed Agency – TTSA, SUA, Chuo cha Olmotonyi na NGOs mf. Acord, Lake Victoria Environment Management Programme – LVEMP).
  2. Kuanzisha miradi ya vitalu vya miti kibiashara – kwa taasisi na watu binafsi kwa kata na vijiji.
  3. Kuhamasisha na kuwawezesha vijana waliomaliza mafunzo kwenye vituo vya ufundi (vocational training) kuanzisha miradi ya ufundi ya kuongeza thamani ya mazao ya miti.

Sekta ya Uvuvi:

  1. Kutoa elimu ya uvuvi kwa maeneo yote ya mwambao wa ziwaVictoria.
  2. Kuanzisha mtandao wa wavuvi.
  3. Kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa vya wavuvi (SACCOS).
  4. Kuendeleza bandari muhimu katika jimbo – Kiloleli, Mwamanyili, Kabita (Nyamikoma) na Kalemela (Lamadi, Kalemela).
  5. Kuhamasisha na kuendeleza ufugaji wa samaki. (Ushauri utapatikana kwa Dr Yohana Budeba/TAFIRI).
  6. Kuanzisha utaalamu wa kuongeza thamani ya mazao ya samaki ikiwemo kukausha na kufunga (packaging) kwa kusafirisha nje ya nchi mf. Congo, Burundi na Kenya.

 

MALENGO YA SEKTA KILIMO NA UFUGAJI JIMBO LA BUSEGA

  1. Kufanya Tathimini ya udongo katika jimbo ili kubaini mazao stahili kwa maeneo mbalimbali (Refer Agricultural Reseach Institute (ARI) – Ukiriguru. Dr.Kileo)
  2. Kuboresha mbegu za mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) kwa kuanzisha kituo cha uhamasishaji (artificial insemination) Nyashimo; na kituo cha madume bora Igalukiro.
  3. Kufundisha na kuhamasisha matumizi ya elimu ya malisho ya mifugo kwa wafugaji na kuanzisha mashamba ya mbegu za malisho kwenye vituo vya mafunzo Jimboni.
  4. Kuanzisha, kuboresha na kulinda maeneo ya malisho ya mifugo zikiwamo ‘’ngitiri” na kutumia mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini (village land use plans).
  5. Kuhamasisha ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa wanawake na vijana na kutengeneza mtandao wa soko. Kutumia uzoefu wa wanawake wa mutukula – kagera (Refer TASAF/Mwamanga/Dr. Mwamuhehe – VIC Iringa). Walianza na kuku 1,000 na katika kipindi cha mienzi9 walikua tayari na mil.97 benki, mwaka mmoja wakawa na mil.120.
  6. Kuanzisha soko la kimataifa la mbuzi mwasamba na maonyasho ya mifugo bora.
  7. Kuimarisha vikundi vya wakulima.
  8. Kuhamasisha shughuli ya unenepeshaji ng’ombe na mbuzi kwa ajili ya soko la kimataifa mf. Comoro, Falme za kiarabu, Kongo, Burundi, Kenya na Sudan.
  9. Kuanzisha ukulima wa mazao mapya mf. Alzeti, dengu, choroko, mbaazi nk.
  10. Kuhamasisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo(agromechanization) kwa kuongeza matumizi ya matrekta, power tillers na plau (Refer Binti Nanai – Mrs.Kaali, Wizara ya kilimo, ARI-Uyole, SUA-Animal science Department, Prof.Abud).
  11. Kufufua kituo cha agromechanization Malili/Igalukilo. (kushirikiana na Roman Catholic – jimbo la Shinyanga).
  12. Kuhamasisha matumizi ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea na mbegu bora kwa kutoa mafunzo kwa wakulima na kuanzisha maduka ya pembejeo kwa kila kata.
  13. Kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo Nyaluhande na Malili.
  14. Kuanzisha ziara za mafunzo za wakulima na viongozi stahili kwenye vyuo vya kilimo, taasisi za utafiti za kilimo, maonyesho ya kilimo nk.
  15. Kuanzisha mtandao wa mabwana shamba na mabwana mifugo jimboni ili kubadilishana mawazo na kuongeza hamasa ya kazi.
  16. Kuanzisha mfumo wa mafunzo endelevu (continuing education/retraining) wa maafisa ugani wa kilimo na mifugo ili kuingiza maarifa mapya ya kilimo na ufugaji jimboni (Refer FAO, UNDP, ASDP)
  17. Kuhamasisha na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwenye Bonde la mto Duma na Bonde la ziwa Victoria. (kutumia uzoefu wa Miradi ya Arumeru, Lushoto, wizara ya kilimo, chuo cha kilimo na kiyuo cha utafiti wa kilimo Ukiriguru na kituo cha umwagiliaji kanda ya ziwa-Nyakato.
  18. Kuanzisha vikosi vya kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji kama vile mabwawa (charco dams) kwenye mito na mabonde yote jimboni. Kata mbili zitaanziwa kama eneo la mfano (pilot project). Vitendea kazi muhimu ni D4 moja na tipper mbili kwa kila kata. Kata za mwanzo ni Kiloleli na Mkula.
  19. Kuanzisha namna ya kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuza mf. Biltong, kuyapima na kupaki kwenye mifuko nk.
  20. Kuanzisha kitengo cha masoko katika ofisi ya mbunge ili kutafuta masoko na bei bora za mazao kwa kushirikiana na mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya. Mpango huu wa kuimarisha kilimo na mifugo utajengwa katika misingi ya kupambana na njaa na kujanisha Busega kwa kuunga mkono mpango wa Taifa wa Kilimo Kwanza.

BUDECO katika Elimu

BUDECO yachangia ujenzi wa madarasa Sh mil 34.7
icon siku ya makabidhiano ya mchango1

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.

°F | °C
Error! Unable to Find Specified Location!