- Kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kijamii (elimu, afya, michezo, maji miundombinu, Kilimo, mifugo, uvuvi, ufugaji nyuki na samaki, fedha, viwanda na biashara) katika wilaya ya Busega.
- Kushiriki katika uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti, usafi wa mazingira na kutoa elimu ihusuyo uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
- Kushiriki katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa kutoa elimu ya kujikinga, ushauri nasaha na kusaidia waathirika km vile wajane, wagane na watoto yatima
- Kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za mauaji ya kikatili dhidi ya vikongwe na walemavu wa ngozi.
- Kutoa elimu ya ujasiliamali ili kujenga ustawi wa wanawake na vijana.
- Kutoa elimu kwa jamii ihusuyo maadili, utamaduni na utu wa Mtanzania.
- Kushirikiana wakati wa shida na raha (msiba, ugonjwa, sherehe n.k)
- Kusaidia na kuhamasisha Elimu ya uraia na utawala bora.
- Kuhamasisha jamii kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya, ukeketaji na unyanyasaji wa kinjisia.
- Kushirikiana na jamii ya Watanzania katika shughuli za maendeleo ya jamii katika sehemu zote palipo na matawi ya BUDECO.
- Kushiriki katika shughuli zingine zote zihusuzo maendeleo na ustawi wa jamii.
Error! Unable to Find Specified Location!