Ijumaa, Julai 05, 2024

Hapo tarehe 16/09/2014 Mwenyekiti wa BUDECO Bw. Joseph Ginhu Masele aliutangazia umma kuwa Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) imepokea vitabu vyenye thamani ya shilingi 5,100,000/= kutoka kwa Mh. Nyambari Chacha Mariba Nyangwine, Mbunge wa Tarime(CCM).

Hii ni mojawapo kati ya mikakati ya kuleta maendeleleo inayoendelea kufanywa na Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (Busega Development Community – BUDECO) katika wilaya ya Busega. Aidha kwa kufanya hivi mheshimiwa Nyangwine alikuwa akitekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa harambee iliyofanywa wakati wa kuasisiwa rasmi kwa jumuiya hii hapo mwaka jana 2013.

Hatimaye siku ya Jumamosi tarehe 20/09/2014 mwenyekiti Bw. Masele aliwakaribisha wana-BUDECO kwenye hafla ya ugawaji wa vitabu kwenye halmashauri ya wilaya ya Busega saa 4 asubuhi. Kama picha zinavyoonesha, zoezi hili lilifanyika kwa mafanikio kama ilivyokuwa imepangwa mbele ya kaimu mkurugezi, mwenyekiti wa halmashauli, walimu wakuu wa shule 6 za srkondari, katibu wa mbunge na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi. Shule za sekondari 6 kati ya shule 17 katika wilaya ya Busega zilizonufaika na mgawo huu ni Ngasamo, Mwamagigisi, Kijereshi, Sogesca na Kabita.

Mlezi wa BUDECO na mbunge wa Busega ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh. Dr. Titus Kamani alitoa shukurani kwa wana-BUDECO kwa kukamilisha zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya jimbo na wilaya kwa ujumla kwa kusema, mvumilivu hula mbivu: "Ng'wibulaga ishing'weng'we. Hatimaye Busega tutafika. Huu ni mfano mzuri sana wa uzalendo." Shukurani nyingi ziende kwa mbunge Mh. Nyambari Nyangwine.

budeco msaada vitabu 2014-09-21 11.39.39
Uongozi wa BUDECO ukikabidhi shehena kubwa ya vitabu kwa halmashauri ya Busega(W)

budeco msaada vitabu 2014-09-21 11.40.30

 

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.

°F | °C
Error! Unable to Find Specified Location!