Karibu kwenye tovuti ya Jumuiya ya BUDECO!
BUDECO ni Shirika lisilo la kiserikali, kidini wala kikabila. Malengo yake yameainishwa katika Katiba ya jumuiya hii. Aidha asasi hii ilianzishwa tarehe 15/Oktoba/2013 kwa lengo la kuchangia shughuli za maendeleo, kuhamasiha na kuijengea uwezo jamii ya Wana-Busega ili kutumia rasilimali zilizopo kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kama ilivyoainishwa katika dira, dhima na madhumuni ya katiba yake.
BUDECO inamilikiwa na kuendeshwa na Wanachama kupitia vyombo vyake. Lengo Kuu ni kuimarisha mshikamano na umoja miongoni mwa wanachama wake pamoja na wanachama wengine wa vyama vya kijamii nchini. Aidha BUDECO inaimarisha uhusiano mzuri baina ya Jamii ya Wanabusega waishio Busega na wale waihio nje ya Busega, pamoja na wafadhili mbalimbali wa asasi hii.
|
|