Ijumaa, Julai 05, 2024

Hapo tarehe 12/09/2014 JUMUIYA ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) ililaani vikali tukio la kuporwa pesa kwa walimu na kubakwa kwa mwalimu wa kike wa shule ya sekondari Kishamapanda iliyoko wilaya ya Busega, mkoani Simiyu.

Tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka huu, ambako watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi waliokubuhu walivamia nyumba ya Mratibu wa Elimu Kata, Samwel Mkumbo na kumpora shilingi milioni 18 kabla ya kwenda kwenye chumba cha mpangaji wake wa kike ambaye pia ni mwalimu na kumpora shilingi 50,000 na kisha kumbaka kwa zamu.

Akisoma tamko ramsi la jumuiya hii mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BUDECO, Bw. Massele Ginhu alisema, tukio hilo ni la kulaaniwa kwa nguvu zote na kila mtu kwani litarudisha nyuma maendeleo ya elimu, kwa kuwa ni moja ya changamoto inayowakabili wilayani humo.

Kufuatia tukio hili uongozi wa BUDECO uliitisha mchango wa pole kwa mwalimu aliyebakwa ambapo shilingi 110,000/= zilichangwa na kukabidhiwa kwa mhanga hapo tarahe 10/09/2014.

  • Habari kamili iliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na redio na magazeti  kama vile: Radio 98.10 FM na gazeti la UHURU, MTANZANIA, MWANANCHI, MSEMA KWELI, na TANZANIA DAIMA.
  • TAMKO RASMI

BUDECO katika Elimu

BUDECO yachangia ujenzi wa madarasa Sh mil 34.7
icon siku ya makabidhiano ya mchango1

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.

°F | °C
Error! Unable to Find Specified Location!