Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Simiyu
Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Simiyu inashughulika na shughuli mbalimbali zinazohusu Viwanda, Biashara, Masoko na Uwekezaji kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Biashara, Sera ya Taifa ya Uwekezaji, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2011/12-2015/16, Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umasikini Awamu ya Pili (MKUKUTA II) na Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda 1996-2020.
Shughuli zinazofanywa ni kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweza kufanikisha Sera, Sheria na Mipango mbalimbali ya kitaifa, kusimamia utekelezaji wa Sheria za Biashara na Viwanda, Kutoa ushauri wa kibiashara kwa wadau mbalimbali, Kuratibu shughuli za usajili wa Leseni za Biashara, Kusimamia mwenendo wa Masoko, Kuhamasisha shughuli za Wajasiriamali, Biashara Ndogo, Kati na Viwanda Vidogo (SME’s), Kuhamasisha na kuvutia Uwekezaji katika maeneo ya Kilimo, Madini, Utalii na Viwanda hususani viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.
Endelea kusoma kwenye Blog rasmi ya Mkoa wa Simiyu: http://simiyuregion.blogspot.com/p/blog-page_28.html
Pakua(download) nyaraka, Fomu na taarifa mbalimbali
- Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara
- Sheria ya Leseni za Biashara na. 25 ya 1972
- Sheria ya Fedha Na. 2 ya 2014
- Sheria ya Makampuni ya 2002
- Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997
- Muongozo wa Kodi(Tax Guide)
- Fursa za uwekezaji Tanzania
- Mwongozo wa Uwekezaji Tanzania
- Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Simiyu
Tovuti Muhimu za Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji