Karibu kwenye tovuti ya Jumuiya ya BUDECO!
BUDECO ni Shirika lisilo la kiserikali, kidini wala kikabila. Malengo yake yameainishwa katika Katiba ya jumuiya hii. Aidha asasi hii ilianzishwa tarehe 15/Oktoba/2013 kwa lengo la kuchangia shughuli za maendeleo, kuhamasiha na kuijengea uwezo jamii ya Wana-Busega ili kutumia rasilimali zilizopo kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kama ilivyoainishwa katika dira, dhima na madhumuni ya katiba yake.
Soma zaidi...
Dar es Salaam, 26/Oktoba/2019
Uongozi wa BUDECO leo hii ukiwakilishwa na Naibu Mwenyekiti Bwana Mashauri Nkonoki na Mtunza Hazina Dr Julius Manyanda na Bwana Mathias Lung'wecha wameshiriki kwenye hafla iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani Jijini Dar-es-Salaam, Mlimani City, kwa ajili ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba 2019.
Aidha uongozi wa BUDECO, shirika ambalo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu umewapongeza sana wanafunzi wane (4) – wavulana watatu na msichana mmoja -- walioshika nafasi muhimu ndani ya kumi (10) bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu.
-- PICHA Wanafunzi wa Busega walioingia kwenye 10 bora kitaifa wakiwa na viongozi wa wilaya jijini Dar es Salaam --
Mheshimiwa mbunge wa Busega, Dr Raphael Chegeni alinukuliwa akisema: “Ni faraja kubwa kwa wana Busega wote ikiwa ni historia kwa ufaulu wa vijana wetu waliomaliza darasa la saba. Kitaifa matokeo yametupa uwepo wa vijana wetu kwenye nafasi muhimu za kitaifa. Napenda kuwapongeza sana wanafunzi hawa walioshika nafasi muhimu ndani ya 10 bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu. Tunataraji hata vijana wetu wa kidato cha nne nao watafanya vizuri.”
Soma zaidi...
Wana-BUDECO, Wana-Busega na Watanzania kwa ujumla tumepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha kijana wetu, Bw. Nelson V. Mabeyo na abiria wengine kilichotokea katika ajali ya ndege huko Seronera hapo Jumatatu, tarehe 23/09/2019.
(c) www.thecitizen.co.tz
Bwana awape faraja familia ya mkuu wa majeshi Tanzania, CDF Venance Mabeyo, ndugu, marafiki na jamaa wote kwa msiba huu mzito.
Kijana wetu mpendwa, mtoto wa mwanachama mwenzetu wa BUDECO, umeondoka wakati taifa zima la Tanzania linakutegemea na lina uhitaji wa taaluma yako na uwepo wako.
Wana BUDECO tunaendelea na mipango ya kushiriki kikamilifu kwa kuwafariji wafiwa katika msimba huu.
Tunaomba Mwenyezi Mungu awape ustahimivu na faraja ya Moyo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
RIP NELSON V. MABEYO. AMINA.
PS:
MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA NDG CDF VENANCE MABEYO ALIYEFIWA NA MTOTO WAKE ITUMWE KWA MPESA, AIRTEL MONEY AU TiGO PESA kwa kutumia namba hizi: 0752 845 357 au 0712 291 400. Majina ya namba hizo ni Mashauri Kanesenese.
Asanteni.
Mwenyetiki wa BUDECO
Bw. Maselle Joseph Ginhu
Soma zaidi...
RM, 01/03/2018
Jumuiya ya Maendeleo ya Wana-Busega waishio nje ya Busega, BUDECO (Busega Development Community) imepongezwa na mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Seif Mwera kwa kutoa mchango wa fedha taslimu Shilingi 34,700,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Busega.
Mchango huu uliwasilishwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 26/02/2018 katika ofisi ya mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya BUDECO Bw. Maselle Joseph Ginhu kwa kushirikiana na mwakilishi wa wanachana waishio karibu na Busega, Dr. Simon Songe.
Mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Mwera akimkabidhi hati ya shukurani Mwenyetiki wa BUDECO Bw. Maselle Joseph Ginhu. Aliyesimama katikati ni Dr Simon Songe.
Katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya mchango huu ambayo ilishuhudiwa pia na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Busega, mkuu wa wilaya Bi. Tano Mwera alinukuliwa akisema:
“Kwa niaba ya wilaya ya Busega nawashukuru sana wana-BUDECO kwa mchango huu wa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya yetu ya Busega.”
Soma zaidi...
Hapo tarehe 12/09/2014 JUMUIYA ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) ililaani vikali tukio la kuporwa pesa kwa walimu na kubakwa kwa mwalimu wa kike wa shule ya sekondari Kishamapanda iliyoko wilaya ya Busega, mkoani Simiyu.
Tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka huu, ambako watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi waliokubuhu walivamia nyumba ya Mratibu wa Elimu Kata, Samwel Mkumbo na kumpora shilingi milioni 18 kabla ya kwenda kwenye chumba cha mpangaji wake wa kike ambaye pia ni mwalimu na kumpora shilingi 50,000 na kisha kumbaka kwa zamu.
Soma zaidi...
Hapo tarehe 16/09/2014 Mwenyekiti wa BUDECO Bw. Joseph Ginhu Masele aliutangazia umma kuwa Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) imepokea vitabu vyenye thamani ya shilingi 5,100,000/= kutoka kwa Mh. Nyambari Chacha Mariba Nyangwine, Mbunge wa Tarime(CCM).
Hii ni mojawapo kati ya mikakati ya kuleta maendeleleo inayoendelea kufanywa na Jumuiya ya Maendeleo ya Wanabusega (Busega Development Community – BUDECO) katika wilaya ya Busega. Aidha kwa kufanya hivi mheshimiwa Nyangwine alikuwa akitekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa harambee iliyofanywa wakati wa kuasisiwa rasmi kwa jumuiya hii hapo mwaka jana 2013.
Soma zaidi...