Wageni karibuni!
Napenda tukumbushane moja ya masharti muhimu katika group hili.
- Group hili ni maalumu kwa members wa Jumuiya ya Maendeleo ya wanabusega (BUDECO). Hivyo michango ya mawazo inayoruhusiwa humu ni ile yenye mlengo wa kuendeleza umoja wetu na Busega yetu.
- Group hili limetengenezwa maalumu kuwa kisima cha mawazo ya maendeleo ya BUDECO na Busega kwa ujumla.
- Group hili limesheheni watu wa aina tofauti, vijana na wazee, viongozi na wasio viongozi. Hivyo Ndani ya group hili hairuhusiwi kabisa michango ya mawazo yenye affiliation za kisiasa.
Kwa wageni mliounganishwa na wenyeji mliomo tuzingatie vigezo na masharti yaliyoainishwa hapo juu.
Ahsanteni.
Imetolewa na Ginhu JM
Mwenyekiti - BUDECO.