Wednesday, July 03, 2024

Wilaya ya Busega yatia fora kwa ufaulu mzuri ndani ya kumi (10) bora kitaifa kwenye mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2019

Dar es Salaam, 26/Oktoba/2019

Uongozi wa BUDECO leo hii ukiwakilishwa na Naibu Mwenyekiti Bwana Mashauri Nkonoki na Mtunza Hazina Dr Julius Manyanda na Bwana Mathias Lung'wecha wameshiriki kwenye hafla iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani Jijini Dar-es-Salaam, Mlimani City, kwa ajili ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba 2019.

Aidha uongozi wa BUDECO, shirika ambalo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu umewapongeza sana wanafunzi wane (4) – wavulana watatu na msichana mmoja -- walioshika nafasi muhimu ndani ya kumi (10) bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu.  

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 3
-- PICHA Wanafunzi wa Busega walioingia kwenye 10 bora kitaifa wakiwa na viongozi wa wilaya jijini Dar es Salaam --

Mheshimiwa mbunge wa Busega, Dr Raphael Chegeni alinukuliwa akisema: “Ni faraja kubwa kwa wana Busega wote ikiwa ni historia kwa ufaulu wa vijana wetu waliomaliza  darasa la saba. Kitaifa matokeo yametupa uwepo wa vijana wetu kwenye nafasi muhimu za kitaifa. Napenda kuwapongeza sana wanafunzi hawa walioshika nafasi muhimu ndani ya 10 bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu. Tunataraji hata vijana wetu wa kidato cha nne nao watafanya vizuri.”

Read more ...

Salamu za rambirambi kwa ndg CDF Venance Mabeyo aliyefiwa na mtoto wake, Bw. Nelson V. Mabeyo, tarehe 23/09/2019

Wana-BUDECO, Wana-Busega na Watanzania kwa ujumla tumepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha kijana wetu, Bw. Nelson V. Mabeyo na abiria wengine kilichotokea katika ajali ya ndege huko Seronera hapo Jumatatu, tarehe 23/09/2019.

Plane+Nelson Mabeyo CITIZEN
(c) www.thecitizen.co.tz

Bwana awape faraja familia  ya mkuu wa majeshi Tanzania, CDF  Venance Mabeyo, ndugu, marafiki na jamaa wote kwa msiba huu mzito.
Kijana wetu mpendwa, mtoto wa mwanachama mwenzetu wa BUDECO, umeondoka wakati taifa zima la Tanzania linakutegemea na lina uhitaji wa taaluma yako na uwepo wako.

Wana BUDECO tunaendelea na mipango ya kushiriki kikamilifu kwa kuwafariji wafiwa katika msimba huu.
Tunaomba Mwenyezi Mungu awape ustahimivu na faraja ya Moyo.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
RIP NELSON V. MABEYO. AMINA.

PS:
MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA NDG CDF VENANCE MABEYO ALIYEFIWA NA MTOTO WAKE ITUMWE KWA MPESA, AIRTEL MONEY AU TiGO PESA kwa kutumia namba hizi: 0752 845 357 au 0712 291 400. Majina ya namba hizo ni Mashauri Kanesenese.

Asanteni.

Mwenyetiki wa BUDECO
Bw. Maselle Joseph Ginhu

Read more ...

Mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Mwera aishukuru jumuiya ya BUDECO kwa mchango wa ujenzi wa madarasa wa Shilingi milioni 34.7

RM, 01/03/2018
Jumuiya ya Maendeleo ya Wana-Busega waishio nje ya Busega, BUDECO (Busega Development Community) imepongezwa na mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Seif Mwera kwa kutoa mchango wa fedha taslimu Shilingi 34,700,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Busega.

Mchango huu uliwasilishwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 26/02/2018 katika ofisi ya mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya BUDECO Bw. Maselle Joseph Ginhu kwa kushirikiana na mwakilishi wa wanachana waishio karibu na Busega, Dr. Simon Songe. 

siku ya makabidhiano ya mchango5 mkuu wa wilaya bi tano akimkabidhi mkiti maselle hati
Mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Mwera akimkabidhi hati ya shukurani Mwenyetiki wa BUDECO Bw. Maselle Joseph Ginhu. Aliyesimama katikati ni Dr Simon Songe.

Katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya mchango huu ambayo ilishuhudiwa pia na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Busega, mkuu wa wilaya Bi. Tano Mwera alinukuliwa akisema:
“Kwa niaba ya wilaya ya Busega nawashukuru sana wana-BUDECO kwa mchango huu wa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya yetu ya Busega.”

Read more ...

Wito kwa wanachama wa BUDECO kuchangia ujenzi wa madarasa kwa shule za Sekondari wilayani Busega

Rejea Tangazo lililotolewa tar 16.12.2017 juu ya Ombi kutoka uongozi wa Wilaya juu ya wito wa kuchangia ujenzi wa madarasa kwa shule za Sekondari.

Ndg wanabusega salamu:

Nimepokea ujumbe wa maandishi na sauti kutoka kwa DC Busega akituomba kushiriki katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha Vijana wetu kujiunga na masomo ya sekondari kwa mwaka 2018.

Tafadhalini  naomba tusome kwa makini andiko lake ili tujadiliane namna ya kushiriki kupitia BUDECO WhatsApp group .icon-icon-comments.

Ahsanteni.

Imetolewa na Ginhu JM
Mwenyekiti - BUDECO.

Read more ...

Angalizo kwa wanaojiunga na BUDECO WhatsApp group

Wageni karibuni!

Napenda tukumbushane moja ya masharti muhimu katika group hili.

  1. Group hili ni maalumu kwa members wa Jumuiya ya Maendeleo ya wanabusega (BUDECO). Hivyo michango ya mawazo inayoruhusiwa humu ni ile yenye mlengo wa kuendeleza umoja wetu na Busega yetu.
  2. Group hili limetengenezwa maalumu kuwa kisima cha mawazo ya maendeleo ya BUDECO na Busega kwa ujumla.
  3. Group hili limesheheni watu wa aina tofauti, vijana na wazee, viongozi na wasio viongozi. Hivyo Ndani ya group hili hairuhusiwi kabisa michango ya mawazo yenye affiliation za kisiasa.

Kwa wageni mliounganishwa na wenyeji mliomo tuzingatie vigezo na masharti yaliyoainishwa hapo juu.

Ahsanteni.

Imetolewa na Ginhu JM
Mwenyekiti - BUDECO.

BUDECO katika Elimu

BUDECO yachangia ujenzi wa madarasa Sh mil 34.7
icon siku ya makabidhiano ya mchango1

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.