Wednesday, July 03, 2024

Dar es Salaam, 26/Oktoba/2019

Uongozi wa BUDECO leo hii ukiwakilishwa na Naibu Mwenyekiti Bwana Mashauri Nkonoki na Mtunza Hazina Dr Julius Manyanda na Bwana Mathias Lung'wecha wameshiriki kwenye hafla iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani Jijini Dar-es-Salaam, Mlimani City, kwa ajili ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la saba 2019.

Aidha uongozi wa BUDECO, shirika ambalo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu umewapongeza sana wanafunzi wane (4) – wavulana watatu na msichana mmoja -- walioshika nafasi muhimu ndani ya kumi (10) bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu.  

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 3
-- PICHA Wanafunzi wa Busega walioingia kwenye 10 bora kitaifa wakiwa na viongozi wa wilaya jijini Dar es Salaam --

Mheshimiwa mbunge wa Busega, Dr Raphael Chegeni alinukuliwa akisema: “Ni faraja kubwa kwa wana Busega wote ikiwa ni historia kwa ufaulu wa vijana wetu waliomaliza  darasa la saba. Kitaifa matokeo yametupa uwepo wa vijana wetu kwenye nafasi muhimu za kitaifa. Napenda kuwapongeza sana wanafunzi hawa walioshika nafasi muhimu ndani ya 10 bora kitaifa, waalimu, wazazi na uongozi wote wa wilaya kwa kuwezesha ufaulu huu. Tunataraji hata vijana wetu wa kidato cha nne nao watafanya vizuri.”

wilaya ya busega yaongoza kwa ufaulu darasa la 7 psle 2019
-- PICHA ufaulu darasa la 7 mwaka 2019 kama ulivyochapishwa na baraza la mitihani --

Naye mlezi wa jumuiya ya BUDECO, akiwakilisha wanachama wengi wa jumuiya Bwana Lameck Kipilyango alinukuliwa akisema: “Ni kweli. Hii ni faraja ya kipeke kwa wilaya yetu. Mbinu zilizotumika kupata ufaulu huu ziimarishwe na kuboreshwa zaidi. Bwana atubariki wote tuliochangia kufikia mafanikio haya.”

Uongozi wa BUDECO kupitia Kamati Tendaji kwa kushirikiana na Kamati ya Mipango ilifanya mpango wa kuwazawadia washindi kwa lengo la kutoa chachu kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri, ambapo viongozi na wawakilishi wa BUDECO waliandaa hafla ndogo ya kuwapongeza vijana na kupata chakula cha pamoja kwenye hoteli ya Golden Pack Sinza. Wanafunzi hawa walikabidhiwa na BUDECO zawadi ya Tsh Elfu 50 na Mathematical set kila mmoja pamoja na Mwalimu bora kutoka Busega. Afisa Elimu Taaluma Bi. Anna Morandi aliyeongozana na watoto waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba alipata fusra ya kutoa neno akifuatiwa na Naibu Mwenyekiti wa BUDECO Bwana Mashauri Nkonoki.

hafla ndogo ya budeco kuwapongeza vijana golden park sinza 2019 10 26 at 16.40.53

Hali kadhalika diwani wa kata ya Nyashimo Mheshimiwa Bi. Mickness Mahela, alinukuliwa akitoa shukurani kwa wadau wa Jukwaa la Nyashimo kwa kusema: "Napenda kutoa pongezi nyingi sana kwenu walimu wetu wote wa Kata ya Nyashimo Shule ya Msingi na Sekondari kwa jitihada zenu za kuhakikisha wanafunzi na watoto wetu wanapata ufaulu mzuri na kuwaandalia maisha yao mazuri ya badae pamoja na familia zao na jamii kwa ujumla. Pongezi za kipekee napenda kuzitoa kwa Walimu wote wa Shule ya msingi Nassa na Nyashimo kwa kuiweka Kata ya Nyashimo, Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu ktk ramani ya kufaulisha wanafunzi 2 ktk kumi bora ya Kitaifa.
Siyo kazi rahisi isipokuwa ni jitihada zaidi zilitumika kwa ushirikiano wa Walimu, Wanafunzi, Wazazi, Wadau na Serikali na hatimaye matokeo yameonekana, Mubarikiwe sana."

Majina ya vijana wetu waliofanya vizuri:

1. Maria Paul Baleke - kutoka Shule ya Msingi ya Nyaruhande
Ameshika nafasi ya 8 kati ya wanafunzi wa kike 10 kitaifa.

2. Busumba Peter Charles - kutoka shule ya msingi Nyashimo.
Ameshika nafasi ya 5 kitaifa kwa shule za serikali. Kwa wavulana ameshika nafasi ya 4 kitaifa.

3. Jonson Goodluck John - kutoka shule ya msingi Nassa.
Ameshika nafasi ya 10 kitaifa. Kwa wavula ameshika nafasi ya 8 kitaifa. Ina maana alizidiwa na wasichana wawili kitaifa.

4. Ngulung'wa Seleman Zacharia - kutoka shule ya msingi Ng'wamagulu.
Kitaifa amekuwa wa 9 na kwa wavulana na wa 7 kitaifa.

5. Mwalimu Minza Ndono Maduka kutoka Shule ya msingi Ijitu Masanza amekuwa msimamizi bora wa mitihani kitaifa.

Hivyo, tunawapongeza vijana wetu pamoja na Mwalimu Minza kwa kuinyanyua Busenga na Simiyu kwa ujumla.

 

Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Maendeleo ya Wana-Busega, BUDECO (Busega Development Community) ilianzishwa rasmi tarehe 15/Oktoba/2013 kwa lengo la kuchangia shughuli za maendeleo, kuhamasiha na kuijengea uwezo jamii ya Wana-Busega ili kutumia rasilimali zilizopo kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kama ilivyoainishwa katika dira, dhima na madhumuni ya katiba yake. Mpaka sasa shirika hili limekuwa mstari wa mbele katika kutoa michango mbalimbali ya kufanikisha hususani sekta ya elimu katika wilaya ya Busega. Kwa mfano mwaka 2018, Jumuiya ya Maendeleo ya Wana-Busega, BUDECO (Busega Development Community) ilipongezwa sana na mkuu wa wilaya ya Busega Bi. Tano Seif Mwera kwa kutoa mchango wa fedha taslimu Shilingi 34,700,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Busega. Na mara nyingi imetoa vitabu kwa ajili ya shule mbalimbali wilayani humo.
Viongozi wa BUDECO wamepiga picha mbalimbali na vijana waliofanya vizuri kwenye tamasha hili la kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri mitihani ya darasa la saba kitaifa.

-- PICHA Photoalbum (itaendelezwa) --

bw nkonoki na bw manyanda wakiongea na mdau wa elimu kutoka wilaya ya busega3
-- PICHA Viongozi wa BUDECO Naibu M/Kiti Bw Mashauri Nkonoki na Mtunza Hazina Dr Julius Manyanda na Bw Mathias Lung'wecha wakiongea na viongozi wa sekta ya elimu wilaya ya Busega kwenye hafla ya leo --

 

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 2 Selemani  Zacharia wa 7 kitaifa
-- PICHA Selemani Zacharia kashika nafasi ya 9 kitaifa kwa shule za serikali na ya 7 kitaifa kwa watoto wa kiume --

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 maria amekuwa wa 8 kitaifa
-- PICHA Maria Balekele kashika nafasi ya 8 kitaifa kwa watoto wa kike--

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 johnson goodluck wa 10 kitaifa
-- PICHA Johnson Goodluck kashika nafasi ya 10 kitaifa kwa shule za serikali na ya 8 kitaifa kwa watoto wa kiume --

mwanafunzi kutoka wilaya ya busega 2019 - busumba na baba yake mwl Peter Charles
-- PICHA Busumba Charles kashika nafasi ya 5 kitaifa kwa shule za serikali na ya 4 kitaifa kwa watoto wa kiume --

 

BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...
BUDECO yawa...

BUDECO katika Elimu

BUDECO yachangia ujenzi wa madarasa Sh mil 34.7
icon siku ya makabidhiano ya mchango1

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.