Friday, July 05, 2024

Rejea Tangazo lililotolewa tar 16.12.2017 juu ya Ombi kutoka uongozi wa Wilaya juu ya wito wa kuchangia ujenzi wa madarasa kwa shule za Sekondari.

Ndg wanabusega salamu:

Nimepokea ujumbe wa maandishi na sauti kutoka kwa DC Busega akituomba kushiriki katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha Vijana wetu kujiunga na masomo ya sekondari kwa mwaka 2018.

Tafadhalini  naomba tusome kwa makini andiko lake ili tujadiliane namna ya kushiriki kupitia BUDECO WhatsApp group .icon-icon-comments.

Ahsanteni.

Imetolewa na Ginhu JM
Mwenyekiti - BUDECO.

Tafadhari rejea mazungumzo yetu kwa njia ya simu. Kuhusiana na uhaba wa vyumba vya madarasa kwa dharura ya sasahivi. wanafunzi waliokosa nafasi  ya kuingia form one ni 1207. Tunahitajika tujenge madarasa 10 kufikia Feb 15. 2018. Hayo madarasa yatagharimu milioni 200. Lamadi 4 Nassa 2. Sogesca 4. Ambapo kila darasa moja litagharimu million 20 kwa ujenzi wa kawaida pamoja na madawati yake. Kama mdau kupitia umoja wenu wa wana Busega tunaomba mchango wenu wa hali na mali. Tunusuru vijana wetu wasome. ukipita huo muda watakuwa wamepoteza haki yao ya msingi. Tunatanguliza shukrani. Mungu awabariki sana. DC BUSEGA.

BUDECO katika Elimu

BUDECO yachangia ujenzi wa madarasa Sh mil 34.7
icon siku ya makabidhiano ya mchango1

Chaki kutoka Maswa, Simiyu

WhatsApp group

Chat na wanaBUDECO papo kwa papo.
BUDECO chat
Tuma taarifa hizi zikiwa pamoja na namba yako ya simu na anuani ya email:
1.Majina yako matatu, 2.Kijiji unachotoka (kata na tarafa), 3. Kwa sasa unaishi wapi, 4. Shuguli unazofanya au unazopanga kufanya na makampuni/mashirika uliyofanyia/unayofanyia kazi (ukipenda lakini)

Tuma kwenye namba hii 0713-982855 na baadaye ukumbini kwa kujitambulisha.