Wana-BUDECO, Wana-Busega na Watanzania kwa ujumla tumepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha kijana wetu, Bw. Nelson V. Mabeyo na abiria wengine kilichotokea katika ajali ya ndege huko Seronera hapo Jumatatu, tarehe 23/09/2019.
(c) www.thecitizen.co.tz
Bwana awape faraja familia ya mkuu wa majeshi Tanzania, CDF Venance Mabeyo, ndugu, marafiki na jamaa wote kwa msiba huu mzito.
Kijana wetu mpendwa, mtoto wa mwanachama mwenzetu wa BUDECO, umeondoka wakati taifa zima la Tanzania linakutegemea na lina uhitaji wa taaluma yako na uwepo wako.
Wana BUDECO tunaendelea na mipango ya kushiriki kikamilifu kwa kuwafariji wafiwa katika msimba huu.
Tunaomba Mwenyezi Mungu awape ustahimivu na faraja ya Moyo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
RIP NELSON V. MABEYO. AMINA.
PS:
MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA NDG CDF VENANCE MABEYO ALIYEFIWA NA MTOTO WAKE ITUMWE KWA MPESA, AIRTEL MONEY AU TiGO PESA kwa kutumia namba hizi: 0752 845 357 au 0712 291 400. Majina ya namba hizo ni Mashauri Kanesenese.
Asanteni.
Mwenyetiki wa BUDECO
Bw. Maselle Joseph Ginhu
- Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na uongozi wa BUDECO kwa kutumia namba za simu hapo juu au kwa barua pepe zilizo kwenye tovuti hii www.budeco.co.tz au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.